Tuhifadhi mazingira!

Si jambo geni kuona, na taka kitupwa ovyo Kazagaa mitoni na, maji yetu kawa sivyo Mitaroni kuachana, tashangaa ikaavyo Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.   Na ufuoni hujasazwa, ndo nazo barabara Taka mekuwa kilazwa, kutatiza hadi bara Mimea nayo kamezwa, taka kote bila dira Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.   Na mifugo kapungua, kwacho kifo … Continue reading Tuhifadhi mazingira!

Advertisements

​Elimu ndio Mwangaza

Waanzia chekechea, hadi kikuu chuoni Mwanga huu wapevua, kwa wote wajitosani Sherehe kuwaletea, kwa wote mahafalini Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha. Wafanya hii dunia, kila mja mwanga pate Ufukara wakimbia, starehe mpaka pate  Usogora takwamia, mikononi mwa wapate Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha. Hekima wanabobea, insi siwasalitini Staarabu waekea, wasomao ubongoni Fikira wazipania, kuzidisha mithalani … Continue reading ​Elimu ndio Mwangaza

​Ngonjera: Dini ipi ya kweli?

​Ngonjera Kuhusu Dini 1YAKOBO Yesu Kristo ni mwanawe, muumba ye Rahamani Hutambuhi i dadawe, maninga ‘ko fumbuani Hadi lini sa takawe, ukweli kuambiweni Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka. FATUMA Yesu huyo si mwanawe, acha kunihadaani Sikiza ndo uambiwe, nta toa sikioni Uongo umejazawe, ndiposa hutambuani Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka. 2YAKOBO Hijabu kavaa … Continue reading ​Ngonjera: Dini ipi ya kweli?

​Siniache wewe wangu

Kajibwaga kitandani, yake shuka kashikani Matoye  kalegezani, mekuwa purukushani Juu kajitokezani, mishipa yake ngozini Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi. Wele wamuoneani, kamganda ye mwilini, Memshika kifuani, hutaki kubandukani Sijasahau pafuni, wamtesa kupumwani Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi. Mapema naraukani, uji kutayarishani Kiamka upateni, mekujazia koponi Pigane na uweleni, ujijazie nguvuni Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi. … Continue reading ​Siniache wewe wangu

Mapenzi

MAPENZI  Mapenzi tele ninayo, kwa hii yangu kalamu Sijasaza kitabuyo, ju za gandana ja gamu Za auni isambayo, ujuzi kwa wenye hamu Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu Mapenzi kutoka moyo, mie si mwanaharamu, Takutunza kwa ijayo, milele siku udumu, We’ umwagapo winoyo, wengi wandaa karamu, Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu. Mapenzi … Continue reading Mapenzi

M-A-M-A

Mola kanizawadia, yuyu huyu mwema kwangu,  Uchovu kavumilia, kubeba uzito wangu,  Kurekebisha tabia, kajukumika kwa zangu,  Shukurani hamumu, nampa nina ninaye.  Amana nakuonea, kutoka moyoni mwangu,  Heshima takupatia, njema iwe aushi'ngu,  Tabasamu kusambaa, litawa jukumu langu,  Shukurani hamumu, nampa nina ninaye.  Mama ni mama tambua, elewa mtima wangu,  Sifa takumiminia, kiwango cha nzima chungu,  Kamwe … Continue reading M-A-M-A

Siasa ni za sasa tu!

Muda nao mewadia, wakwenda uchaguzini Wengi nao taridhia, hadi vijitongojini Agosti mekaribia, na wema tuchagueni Siasa ni za sasa tu! Usihadaiwe. Sikubali kupigia, kelele wako pinzani Wala kumkaripia, kwa hatari taletani Maovu yatakutia, yako nafsi gerezani Siasa ni za sasa tu! Usihadaiwe. Meanza kukaribia, tangu ianze kampeni Harambee kuchangia, ndo zako hukosekani Wajinga wapumbazia, wajanja … Continue reading Siasa ni za sasa tu!

Mola tunusuru!

Mchangani kazagaa, kelele wapaza kwote, Mke kapika dagaa, bora yake usitete, Vitambara ndo kavaa, iweje uwe Dangote? Ulevi tatumaliza, Mola tunusuru!   Wanena kama shujaa, ili watu sikusute, Kwetu sisi kunyamaa, midomo kaziba sote, Harufu kama ya baa, wapeleka kwako yote, Ulevi tatumaliza, Mola tunusuru!   Hadhi yako washushaa, takungoja ujipate, Ukomeshe nyanyapaa, wabana pia … Continue reading Mola tunusuru!