Hatujanaswa na Utandabui!

WATOTO:  Tumechachawizwa sisi, sisi ni wa sasa baba Twaishi haya ya kazi, maisha yenye akiba Twachezea zatu basi, tandawazi watubeba Kamwe si hatujanaswa, na huu utandabui.   BABA: Nyinyi ni bure bilashi, kila muda mwapumbazwa Kila sekunde na rashi, zenu huko mwakimbizwa Na ja vizuu mwaishi, hamna la kusikizwa Ala! Fumbueni mato, mfuate zetu nyayo. … Continue reading Hatujanaswa na Utandabui!

Advertisements

Dunia Kigeugeu 

Kweli mie naumia, maisha ya nani nami? Yote haya napitia, yanijaa majonzi mi, Malazini nalilia, insi sinione mimi, Dunia kigeugeu, ikanibadilikia. Malenga kujionea, haya mi sikujawahi, Sasa yakhe naumia, uchungu wa kukirihi, Mtima wangu kajaa, lalama zisizo sihi, Dunia kigeugeu, ikanibadilikia. Masaibu yabishaa, alfajiri mlangoni, Ninangu kagonjekaa, hayo ya niatuani, Hakuna za kulipaa, mikwanja zahanatini … Continue reading Dunia Kigeugeu