Uncategorized

Tuhifadhi mazingira!

Si jambo geni kuona, na taka kitupwa ovyo

Kazagaa mitoni na, maji yetu kawa sivyo

Mitaroni kuachana, tashangaa ikaavyo

Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.

 

Na ufuoni hujasazwa, ndo nazo barabara

Taka mekuwa kilazwa, kutatiza hadi bara

Mimea nayo kamezwa, taka kote bila dira

Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.

 

Na mifugo kapungua, kwacho kifo kiso haki

Kawa gofu kupigia, mizoga imehakiki

Ndege hewa kupepea, meadimika kindaki

Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.

 

Vundo usotamanika, ndio pambio ya siku

Bahari imechafuka, osha tuna bila duku

Waama kumechafuka, hata macho yanashuku

Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.

 

Taka dhahabu tosha, manufaa tele nayo

Ujuzi  ambatanisha,  plastiki tuko nayo

Na viwanda tawekesha, ajira ndo wapatayo

Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.

 

Maji ndo yawa majini, vya majini Bolti kawa

Watoweka stakimuni, wavuvi kapa waiwa

Maji geuzwa sumuni, uwele tukavamiwa

Tupe taka ifaavyo, tuhifadhi mazingira.

 

Leave a comment