​Elimu ndio Mwangaza

Waanzia chekechea, hadi kikuu chuoni

Mwanga huu wapevua, kwa wote wajitosani

Sherehe kuwaletea, kwa wote mahafalini

Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha.

Wafanya hii dunia, kila mja mwanga pate

Ufukara wakimbia, starehe mpaka pate 

Usogora takwamia, mikononi mwa wapate

Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha.
Hekima wanabobea, insi siwasalitini

Staarabu waekea, wasomao ubongoni

Fikira wazipania, kuzidisha mithalani

Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha.
Insi wakutegemea, fanye yako madhubuti

Akili ndio huzaa, ndo mawazo kawa dhati

Ghorofa kuwajengea, kwa yako we mikakati

Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha.
Wote wanatarajia, miujiza kuonayo

Eti ya kuandikia, na kusoma kitabuyo

Sauti kutamkia, ala ni tofautiyo

Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha.
Elimu twasherekea, ujio ‘ko maishani 

Hakika takutendea, haki kutoka mwanzoni

Tija utajivunia, wewe ukiwa kanuni

Elimu ndio mwangaza, yakuboresha maisha.
Stephen Mburu

“Malenga wa Michepuko”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s