Uncategorized

​Ngonjera: Dini ipi ya kweli?

​Ngonjera Kuhusu Dini

1YAKOBO

Yesu Kristo ni mwanawe, muumba ye Rahamani

Hutambuhi i dadawe, maninga ‘ko fumbuani

Hadi lini sa takawe, ukweli kuambiweni

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.

FATUMA

Yesu huyo si mwanawe, acha kunihadaani

Sikiza ndo uambiwe, nta toa sikioni

Uongo umejazawe, ndiposa hutambuani

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.
2YAKOBO

Hijabu kavaa wewe, gurunedi wafichani

Na kanzu  zizingatiwe, bastola zabebeani

Lolote baya na liwe, nyie ndio watendani

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.

FATUMA

Mpumbavu na  usiwe, hatufichi hata pini

Kanzu niza zamaniwe, tena walahi dhamani

Lolote tusingiziwe, wema sisi kutendani

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.
3YAKOBO

Sauti na  mpaziwe, Osama Bin vitendoni

Mbona sisi tuuliwe, na wenye uhayawani

Nyote mfuatiliwe, hadi yote mashimoni

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.

FATUMA

Jioni tuadhiniwe, Yakobo wajichoshani

Magaidi na wenziwe, wote sio wenzetuni

Walahi hadi mwishowe, watachoka tafuteni 

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.
4YAKOBO

Twapagawa na kiwewe, nyie mwatutishiani

Uislamu upigiwe, na mifano vitabuni 

Hatutaki hao mwewe, waua bila hilani

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.

FATUMA

Mkuki chungu kwa nguruwe, vurugu nazuiani

Dini ni yako huruwe, yaache ya mifanoni,

Duniani kuguriwe, ndo kuishi kina nani? 

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.
5YAKOBO

Nakubaliana nawe, meanza ona kanani

Mimi tangu nizaliwe, sijajua ukwelini,

Habari zinyunyiziwe, kwa wengine asilani

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.

FATUMA

Dini na zifurahiwe, silete vizingitini

Umoja na uenziwe, hadi watoka hindini

Kwa kweli tusiletewe, ya makuu kuvunjani 

Dini sio hoja kamwe, aabudiwe Rabuka.

 

2 thoughts on “​Ngonjera: Dini ipi ya kweli?”

Leave a comment