​Siniache wewe wangu

Kajibwaga kitandani, yake shuka kashikani

Matoye  kalegezani, mekuwa purukushani

Juu kajitokezani, mishipa yake ngozini

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Wele wamuoneani, kamganda ye mwilini,

Memshika kifuani, hutaki kubandukani

Sijasahau pafuni, wamtesa kupumwani

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Mapema naraukani, uji kutayarishani

Kiamka upateni, mekujazia koponi

Pigane na uweleni, ujijazie nguvuni

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Hamadi i kibindoni, mwanao ni boritini

Mbele yake Rahamani, mimi hapa naapani

Ile mwisho sekundeni, ndio ntaondokani

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Tangu  u uchipukani, bashasha katowekani

Simanzi kanijazani, kaghubika mtimani

Sijui nitazameni,  yeyote  kuniauni

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Tangu wangu utotoni, njema ukanifunzani

Kuzishika viganjani, siha njema aushini

Sitosahau kamweni, nina ninaye ninani

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Ja takumiminiani, sifa nazo ni teleni

Kwakuwa hazimo habani, hata kiwa malazini

Uso wako tanaani, waleta matumaini

Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi.
Stephen Mburu

“Malenga wa Michepuko”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s