Mapenzi

MAPENZI 
Mapenzi tele ninayo, kwa hii yangu kalamu

Sijasaza kitabuyo, ju za gandana ja gamu

Za auni isambayo, ujuzi kwa wenye hamu

Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu
Mapenzi kutoka moyo, mie si mwanaharamu,

Takutunza kwa ijayo, milele siku udumu,

We’ umwagapo winoyo, wengi wandaa karamu,

Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu.
Mapenzi si kibogoyo, yatafuna si kuchumu,

Daima ya malizayo, upweke wangu kaimu,

Na mengi matamaniyo, moyoni ‘ngu yatadumu,   

Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu.
Mapenzi tele ninayo, heshima kwako tadumu,

Maneno uandikayo, kitabuni ya muhimu,

Hadi karne ijayo, takuwa yao sehemu,

Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu.
Mapenzi tele ninayo, kwa kitabu na kalamu,

Merudia  itoshayo, na sitotaka kusumu,

Kwa mirefu misambayo, na sazuka  ghulamu,

Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu.
STEPHEN MBURU

‘Malenga wa Michepuko’

Advertisements

2 thoughts on “Mapenzi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s