Dunia Kigeugeu 

Kweli mie naumia, maisha ya nani nami?
Yote haya napitia, yanijaa majonzi mi,

Malazini nalilia, insi sinione mimi,

Dunia kigeugeu, ikanibadilikia.

Malenga kujionea, haya mi sikujawahi,

Sasa yakhe naumia, uchungu wa kukirihi,

Mtima wangu kajaa, lalama zisizo sihi,

Dunia kigeugeu, ikanibadilikia.

Masaibu yabishaa, alfajiri mlangoni,

Ninangu kagonjekaa, hayo ya niatuani,

Hakuna za kulipaa, mikwanja zahanatini ,

Dunia kigeugeu, ikanibadilikia.

Yakhe mie nashang’aa, jambo sina la kufanya,

Yangu sasa taduwaa, elimu ya kubambanya,

Hio karo nakosaa, mi sijui la kufanya,

Dunia kigeugeu, ikanibadilikia.

Swahibu kanipotea, nimebaki peke yangu,

Maisha yanidokoa, nayatizama mawingu,

Msaada watokea, huko aliko ye Mungu,

Dunia kigeugeu, ikanibadilikia.

Stephen Mburu

‘Malenga wa Michepuko’.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s