​Siniache wewe wangu

Kajibwaga kitandani, yake shuka kashikani Matoye  kalegezani, mekuwa purukushani Juu kajitokezani, mishipa yake ngozini Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi. Wele wamuoneani, kamganda ye mwilini, Memshika kifuani, hutaki kubandukani Sijasahau pafuni, wamtesa kupumwani Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi. Mapema naraukani, uji kutayarishani Kiamka upateni, mekujazia koponi Pigane na uweleni, ujijazie nguvuni Siniache wewe wangu, mauti isikuwahi. … Continue reading ​Siniache wewe wangu

Advertisements

Mapenzi

MAPENZI  Mapenzi tele ninayo, kwa hii yangu kalamu Sijasaza kitabuyo, ju za gandana ja gamu Za auni isambayo, ujuzi kwa wenye hamu Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu Mapenzi kutoka moyo, mie si mwanaharamu, Takutunza kwa ijayo, milele siku udumu, We’ umwagapo winoyo, wengi wandaa karamu, Wewe ni wangu lazizi, tamwaya penzi hamumu. Mapenzi … Continue reading Mapenzi

Dunia Kigeugeu 

Kweli mie naumia, maisha ya nani nami? Yote haya napitia, yanijaa majonzi mi, Malazini nalilia, insi sinione mimi, Dunia kigeugeu, ikanibadilikia. Malenga kujionea, haya mi sikujawahi, Sasa yakhe naumia, uchungu wa kukirihi, Mtima wangu kajaa, lalama zisizo sihi, Dunia kigeugeu, ikanibadilikia. Masaibu yabishaa, alfajiri mlangoni, Ninangu kagonjekaa, hayo ya niatuani, Hakuna za kulipaa, mikwanja zahanatini … Continue reading Dunia Kigeugeu