Kuwa mume ama mke, Rabuka katujalia Na mipango teketeke, yeye katuandalia Kamwe usiiteleke, aliyokuchagulia Yarabi Mola twokoe, Dunia imepasuka.
Mume na aoe mke, Rabuka katuamrisha
Ila mke yu na mke, kitendo cha kupotosha
Aibu kwa toto jike, kwa anayowasilisha
Yarabi Mola twokoe, Dunia imepasuka.
Ndume naye sisazike, kwa yake kuabisha
Ushoga na usitike, da! tabia yapotosha
Wavyele wawajibike nyendo hii yapotosha
Yarabi Mola twokoe, Dunia imepasuka.
Jamii na igutuke, mema tuishi maisha
Kiona mui sivuke, letu kumrekebisha
Wala simpige teke, lengo letu kuboresha
Yarabi Mola twokoe, Dunia imepasuka.
Stephen Mburu
Malenga wa michepuko
Iko sawa
LikeLiked by 1 person
Kazi Njema Malenga.Shukran! Kwa Habari Kemkem!
LikeLiked by 1 person
Kazi nzuri sana, malenga Mburu. Nimeelimika na kuburudika. Endelea kutia fora
LikeLiked by 1 person
Nashukuru sana ndugu. Inshallah ntabidiika zaidi
LikeLiked by 1 person