Siasa ni za sasa tu!

Muda nao mewadia, wakwenda uchaguzini Wengi nao taridhia, hadi vijitongojini Agosti mekaribia, na wema tuchagueni Siasa ni za sasa tu! Usihadaiwe. Sikubali kupigia, kelele wako pinzani Wala kumkaripia, kwa hatari taletani Maovu yatakutia, yako nafsi gerezani Siasa ni za sasa tu! Usihadaiwe. Meanza kukaribia, tangu ianze kampeni Harambee kuchangia, ndo zako hukosekani Wajinga wapumbazia, wajanja … Continue reading Siasa ni za sasa tu!

Advertisements

Mola tunusuru!

Mchangani kazagaa, kelele wapaza kwote, Mke kapika dagaa, bora yake usitete, Vitambara ndo kavaa, iweje uwe Dangote? Ulevi tatumaliza, Mola tunusuru!   Wanena kama shujaa, ili watu sikusute, Kwetu sisi kunyamaa, midomo kaziba sote, Harufu kama ya baa, wapeleka kwako yote, Ulevi tatumaliza, Mola tunusuru!   Hadhi yako washushaa, takungoja ujipate, Ukomeshe nyanyapaa, wabana pia … Continue reading Mola tunusuru!